Huko Kenya hatma ya wanamichezo 20 nchini humo haijulikani baada ya kupigwa marufuku na Shirika la kupambana na matumizi ya madawa ya kusisimua misuli ADAK nchini humo. Jacob Safari amezungumza na mwanamichezo kutoka pwani ya nchi hiyo katika mji wa Mombasa Anthony Aroshee na anaanza kwa kueleza hasa kilichopelekea hatua hiyo kuchukuliwa.