Tunataka kufahamu ni dhana tu au ni kweli kuwa wanaume walio wengi wanatishika na wanawake waliowazidi kielimu au kimapato. Watajichanganya nao, kunywa vinywaji pamoja na hata kuvutiwa nao, lakini linapokuja swala la mahusiano wanasema ni moto wa kuotea mbali. Ikiwa huo ndio ukweli, basi nani wa kulaumiwa, wanawake au wanaume?