Wanawake na mitindo mipya ya nywele
3 Desemba 2015Matangazo
Alicia Keys na Oprah Winfrey wana nini kinachowafananisha? Wote wawili wana nywele ambazo sio zao, wote wanapenda kutengeneza nywele wakitzumia nywele za kubandika au mawigi. Mada hii ya staili za nywele kwa wanawake walio na nywele za kiafrika kwa kawaida huigizwa kutoka kwa wanawake wa Magharibi. Hii inawafanya wanawake wengi wa kiafrika kulazimika kufanya mabadiliko fulani katika nywele zao, ama kuweka dawa au kusuka nywele ghali, hii inaumiza na hata kuchukuwa muda wao mwingi. Wanawake wa Ivory Coast wapigia debe mitindo ya nywele za asilia.