Waandishi habari nchini Kongo wamegoma kutangaza hii leo, wakipinga kupandishwa kwa bei ya internet nchini humo. Kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa makampuni ya simu yamepandisha bei kwa asilimia 100%, yakidai serikali inawabughudhi katika ulipishaji wa kodi ya mauzo.