Wanne wauawa, Carter Center washuku matokeo ya uchaguzi
11 Desemba 2011Mjini Kinshasa polisi waliripotiwa kuwazingira vijana waliokuwa wakipinga matokeo hayo. Watu kadhaa pia wamekamatwa.
Wakati huo huo, kituo cha waangalizi wa uchaguzi cha Marekani, Carter Center, kimesema idadi ya waliojitokeza kupiga kura katika ngome za rais wa sasa, Joseph Kabila, ilikuwa kubwa mno, huku kura kadhaa zikiwa hazikuhesabiwa katika ngome za mgombea wa upinzani, Etienne Tshisekedi. Kituo hicho kimesema kuwa ukiukwaji wa taratibu ambao haukufafanuliwa ulisababisha kutozingatiwa matokeo ya karibuni vituo 2000.
Ijumaa iliyopita, Tume ya Uchaguzi ilitangaza ushindi wa asilimia 49 wa Rais Kabila, huku Tshisekedi akipata asilimia 32. Bado kuna fursa ya kukata rufaani katika mahakama kuu. Ijumaa iliyopita Tshisekedi alitoa mwito pawepo utulivu.