Waokoaji wawatafuta manusura wa kimbunga kisiwani Mayotte
17 Desemba 2024Inahofiwa mamia hadi maelfu ya watu huenda wamepoteza maisha. Kimbunga Chido kilipiga eneo kubwa la kisiwa cha Mayotte kilicho chini ya Ufaransa na kusababisha uharibifu usio na mfano wa majengo, miundombinu ya nishati na mawasiliano pamoja usambazaji huduma muhimu hasa maji majumbani.
Uharibifu huo umefanya iwe vigumu kuyafikia maeneo mengi ya kisiwa hicho, na kaimu waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bruno Retailleau, amesmea itachukua siku kadhaa kufahamu kwa uhakika idadi ya vifo ambayo amekiri "itakuwa kubwa"
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa aliitisha kikao cha dharura cha baraza lake la mawaziri hapo jana kujadili hali ya Mayotte na ameahidi kukitembelea kisiwa hicho mnamo siku zinazokuja. Vilevile kiongozi huyo ametangaza siku moja ya maombolezo ya kitaifa kufuatia janga hilo.