1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. India kupewa na Marekani vifaa na ujuzi wa kinuklia.

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBec

Marekani na India zimekamilisha majadiliano juu ya makubaliano ya ushirikiano wa kinuklia. Makubaliano hayo , yaliyoidhinishwa na baraza la mawaziri la India mapema wiki hii, yataruhusu India kuweza kupata mafuta ya kinuklia kutoka Marekani pamoja na vifaa kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 30, hata kama India imekataa kujiunga na mkataba wa kutoruhusu kusambaa kwa silaha za kinuklia na imefanya majaribio ya silaha za kinuklia.

Wakati akitangaza makubaliano hayo jana Ijumaa , waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice hakutoa taarifa zaidi za kile kinachoitwa makubaliano ya 123, ambayo yanaweza kwenda umbali zaidi ya masharti yaliyoidhinishwa na baraza la Congress. Wabunge wametishia kuzuwia makubaliano hayo iwapo yatakiuka vipengee vya tahadhari ili kuzuwia matumizi ya kijeshi ya teknolojia ya kinuklia.