1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: India yasema haitaendeleza teknolojia hatari ya nuklia

20 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEsr

Waziri mkuu wa India Manmohan Singh ameihakikishai Marekani kwamba nchi yake haitasambaza teknolojia hatari ya nuklia. Katika hotuba yake kwa bunge la Marekani, Singh aliita India, ambayo ina miliki nishati ya nuklia, kuwa taifa lenye wajibu mkubwa.

Ameongeza kusema atayafanya kila awezalo kuboresha mahusiano kati ya India na Marekani hususan katika vita dhidi ya ugaidi wla kimataifa, ukimwi, kuendeleza demokrasia na kuendeleza raslimali za nishati.