1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Korea Kaskazini yafanya jaribio la kombora

1 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFHd

Afisa mwandamizi wa Ikulu ya Marekani leo hii amesema Marekani inafuatilia kwa makini matukio nchini Korea Kaskazini kufuatia taarifa kwamba serikali ya nchi hiyo imefyatuwa kombora la masafa mafupi kwenye bahari ya Japani.

Andrew Card amesema Korea Kaskazini imewahi kufanya majaribio ya makombora hapo kabla na kwamba hii sio mara ya kwanza kuwepo kwa madai ya kufanya majaribio ya makombora. Afisa huyo amesema wanajuwa nini nia yao.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Kyodo nchini Japani nchi hiyo ilijulishwa juu ya jaribio hilo la kombora na jeshi la Marekani na kwamba mawaziri wa nchi hiyo wametakiwa kuwa katika hali ya tahadhari.

Imeripotiwa kwamba kombora hilo lilifyatuliwa leo hii kutoka mwambao wa mashariki wa Korea Kaskazini na kusafiri kama kilomita 100 hadi lilipoanguka baharini.