1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Korea ya kaskazini kujaribu silaha za kinuklia.

5 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5t

Marekani imesema kuwa haitaivumilia Korea ya kaskazini yenye silaha za kinuklia.

Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Chris Hill amewaambia waandishi wa habari mjini Washington kuwa Korea ya kaskazini ni lazima ichague hali bora ya baadaye ama kuwa na silaha za kinuklia.

Korea ya kaskazini , ambayo inadai kuwa na silaha za kinuklia, imesema mapema wiki hii kuwa inampango wa kufanya majaribio ya mwanzo ya silaha hizo.

Wizara ya mambo ya kigeni ya China , ambayo ni mshirika mkubwa wa karibu wa Korea ya kaskazini, imetoa rai ya kuvumiliana.