1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Marekani na Korea ya kaskazini zaitaka Korea ya kaskazini kurejea katika meza ya majadialiano.

11 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF4p

Rais wa Marekani George W. Bush na rais wa Korea ya kusini Roh Moo-hyun wameitaka Korea ya kaskazini kurejea katika mazungumzo kuhusu mpango wake wa silaha za kinuklia.

Baada ya kukutana katika ikulu ya Marekani, marais hao waliweka kando tofauti zao katika kulielekea tatizo hilo.

Marekani inataka zichukuliwe hatua za kutokubembeleza dhidi ya Korea ya kaskazini na inadai zionekane hatua kabla ya kutoa zawadi ya aina yoyote kwa nchi hiyo.

Korea ya kusini inataka kutumia zaidi njia ya mazungumzo.

Korea ya kaskazini imeonesha nia hivi karibuni ya kurejea katika mazungumzo ambayo iliyasusia mwaka mmoja uliopita.

Lakini pia inaendelea kuzungumzia kuhusu mlundiko wa mabomu yake ya kinuklia na nia yake ya kutengeneza mabomu mengine zaidi.