1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yaitaka Korea Kazkazini kurudi katika mazungumzo

10 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG91

Marekani imeihimiza Korea Kazkazini kurejea katika mazungumzo ya mataifa sita juu ya mpango wake wa kinyuklia.

Kufuatia mazungumzo yake na waziri wa mambo ya kigeni wa Japan, Taro Aso, naibu waziri anayeshughulikia maswala ya Asia Mashariki wa Marekani, Christopher Hill, ameonya Korea Kazkzini inalazimika kuchagua kati ya kuendelea kutengwa na jamii ya kimataifa na kujiunga na jumuiya hiyo.

Marekani inaunga mkono azimio lililowasilishwa na Japan kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka Korea Kazkazini iwekewe vikwazo kwa kufanya majaribio ya makombora yake ya masafa marefu. China na Urusi, ambazo zina kura ya turufu, zinalipinga azimio hilo.

Wakati huo huo ujumbe wa maofisa wa China umewasili leo nchini Korea Kazkazini kujaribu kuishawishi irejee katika mazungumzo ya mataifa sita.