Washington. Mpango wa kufunga vinu vya kinuklia vya Korea unakwenda vizuri.
19 Machi 2007Mjumbe wa Marekani katika majadiliano ya kinuklia Christopher Hill amesema kuwa makubaliano yaliyofikiwa na mataifa sita juu ya kufunga mpango wa silaha za kinuklia wa Korea ya kaskazini unakwenda kwa mujibu ulivyopangwa.
Hill amesema kuwa washiriki katika mazungumzo hayo mjini Beijing wamefikia muafaka katika masuala muhimu ya makubaliano ya Februari 13 ya kufunga mpango huo wa kinuklia.
Hii ni pamoja na kufunga kinu kikuu cha kinuklia cha Korea ya kaskazini na suala la udhibiti kupitia shirika la kimataifa la nishati ya Atomic.
Hill alikuwa akizungumza baada ya siku ya pili ya matayarisho ya mjadala kabla ya mazungumzo kamili ya nchi sita juu ya utekelezaji wa makubaliano hayo ya kinuklia, ambayo yanaanza leo Jumatatu. Makubaliano yatahakikisha Korea ya Kaskazini inapata msaada wa nishati pamoja na misaada mingine baada ya nchi hiyo kufunga kabisa mpango wake wa kinuklia.