Washington: Waziri mkuu wa India analihutubia bunge la Marekani
19 Julai 2005Matangazo
Waziri mkuu Manmohan Singh wa India amelihutubia baraza la wawakilishi na Senate ya Marekani hii leo, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu huko Washington. Jana alifanya mazungumzo katika Ikulu na rais George Bush. Viongozi hao wawili walizungumzia masuala ya kupanuliwa biashara kati ya nchi zao mbili na kuupiga vita ugaidi. Rais Bush alisema mkutano huo uliashiria kile alichokiita mafungamano yanayozidi ya ushirikiano baina ya Marekani na India.