1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Waziri mkuu wa India ziarani nchini Marekani.

19 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEt9

Waziri mkuu wa India Bwana manmohan Singh amekuwa na mazungumzo katika ikulu ya Marekani na rais George W. Bush.

Viongozi hao wawili wamejadiliana kuhusu upanuzi wa uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi.

Bwana Bush amesema kuwa mkutano huo unaakisi kile alichokiita ukuaji wa mahusiano ya ushirikiano kati ya Marekani na India.

Hii leo Bwana Singh anatarajiwa kukihutubia kikao cha pamoja cha bunge la Marekani , kitu ambacho ni viongozi wachache tu wa nje ambao wameweza kupewa nafasi hiyo tangu Bush kushika madaraka hapo Januari 2001.