1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Zoellick aidhinishwa kuwa rais wa benki ya dunia

26 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoD

Magavana wa bodi ya benki ya dunia wamepiga kura kumuidhinisha rasmi mmarekani, Robert Zoellick, kuwa rais wa benki hiyo. Zoellick, mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani na mjumbe wa maswala wa kibiashara, anatarajiwa kuanza kazi yake Jumapili ijayo.

Uteuzi wake haujasababisha mgawanyiko kama ilivyokuwa wakati wa kuteuliwa rais aliyeondoka, Paul Wolfowitz.

Wolfowitz alikubali kung´atuka mwezi uliopita baada ya jopo maalumu kumpata na makosa ya kuvunja sheria za benki ya dunia kwa kumpandisha cheo na kumuongezea mshahara mpenzi wake, Shaha Riza, yapata miaka miwili iliyopita.

Robert Zoellick anakabiliwa na kibarua kigumu cha kujenga uaminifu katika benki ya dunia kufuatia kashfa ya Wolfowitz iliyoiharibia sifa benki hiyo.