WASHINGTON.Marekani yashinikiza hatua kali dhidi ya Korea Kaskazini
12 Oktoba 2006Marekani imesema itashinikiza adhabu kali kwa Korea Kaskazini baada ya jaribio lake la nyuklia wiki hii.
Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa John Bolton anapanga kuandaa muswada katika baraza la usalama la umoja huo vikiwemo vikwazo kamili vya silaha na usafiri.
China mshirika wa karibu wa Korea Kaskazini imekubali nchi hiyo iwekewe vikwazo vya kiwango fulani lakini bila ya kitisho cha matumizi ya nguvu.
Rais Bush wa Marekani amesema ana nia ya kuendelea kusaka suluhisho la kidiplomasia katika mzozo huo lakini amelikataa tena takwa la Korea Kaskazini kutaka paweko mazungumzo ya ana kwa ana na Marekani.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limemaliza mkutano wake bila makubaliano yoyote juu hatua zitakazochukuliwa dhidi ya Korea Kaskazini.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan ameitaka Korea kaskazini kuacha kuitumbukiza nchi hiyo katika mzozo zaidi.
O ton….Ijapokuwa Baraza la Usalama la umoja wa mataifa halikufanikiwa kupata makubaliano juu ya hatua dhidi ya Korea Kaskazini…nina imani kubwa hatua muafaka zita afikiwa hivi karibuni dhidi ya nchi hiyo.