Sekta ya filamu ya nchini Ethiopia hutengeneza tamthilia za kimapenzi za vichekesho kwa ajili ya televisheni. Vijana wachache kati ya waandaa filamu hubahatika kupata nafasi ya kujiunga katika Chuo cha Blue Nile ambapo hujifunza jinsi ya kutengeneza filamu zinazoonyeshwa kwenye majumba ya sinema kwa kutumia bajeti ndogo.