JamiiNigeria
Watoto 35 wapoteza maisha kwenye mkanyagano Nigeria
20 Desemba 2024Matangazo
Mkasa huo ulitokea katika shule ya sekondari ya Kiislamu ya jimbo la kusini magharibi la Oyo, ambako maelfu ya wageni walikuwa wamehudhuria tamasha la kabla ya Krismasi.
Msemaji wa polisi ya eneo hilo Osifeso Adewale amesema watu wanane akiwemo mwalimu mkuu wa shule hiyo, wamekamatwa kuhusiana na ajali hiyo.
Polisi inaamini mkanyagano ulianzia wakati waandaaji walipoanza kugawa chakula na vinywaji. Matukio ya watu kukanyagana yamewahi kutokea katika siku za nyuma katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi na hasa kwenye hafla ambazo chakula cha hutolewa.