1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto milioni 6 wakabiliwa na njaa pembe ya Afrika

27 Januari 2017

Watoto milioni 6.5 wanakabiliwa na kitisho cha njaa, utapiamlo na kifo katika maeneo katia mataifa ya Somalia, Ethiopia na Kenya, limesema shirika la hisani wakati ambapo mvua za machipukopia zikitarajiwa kuwa mbaya.

https://p.dw.com/p/2WWb9
Hunger Dürre Kinder Afrika
Picha: picture-alliance/dpa/S. Morrison

Shirika la Save the Children limesema katika taarifa kuwa kukosekana mfululizo kwa mvua kumewatumbukiza katika mgogoro watu milioni 15 katika mataifa hayo matatu, na kuwafanya wahitaji msaada, kwa sababu mifugo yao inakufa na kuna uhaba mkubw wa maji.

"Hali ya watoto wanaoteseka tayari na familia nchini Somalia, Ethipia na Kenya itazidi kuwa mbaya - na kuwaacha mamilini katika hatari ya kukumbw ana njaa, na hata kifo, alismea mkurugenzi wa shirika hilo nchini Ethiopia, John Graham. Wataalamu wanatabiri kuwa msimu ujao wa mvua utaleta mvua za chini ya kiwango katika eneo hilo.

Watoto karibu 500,000 tayari wanakabiliwa na utapiamlo mbaya, ilisema Save the Children, hili likimaanisha kwamba wako hatarini kufa bila msaada wa dharura. Wafadhili, viongozi wa kisiasa na katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wanakutana katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU) unaofunguliwa siku ya Jumatatu nchini Ethiopia.

Symbolbild zum Welthunger Bericht Mädchen aus Somalia
Mtoto anaekabiliwa na utapiamlo nchini Somalia akiwa hospitali mjini Mogadishu.Picha: Abdifitah Hashi Nor/AFP/Getty Images

Guterres ndiye alikuwa mkuu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR wakati wa mgogoro wa njaa nchini Somalia mwaka 2011, ambapo watu 260,000 walikufa kutokana na ukame, mgogoro na marufuku dhidi ya kupelekwa msaada wa chakula katika maeneo yanayoshikiwa na kundi la waasi la Al-Shabaab.

UN yaonya juu ya hatari ya njaa Somalia

Umoja wa Mataifa ulionya mwezi huu kwamba Somalia, ambayo imeharibiwa na miongo zaidi ya miwili ya vita, iko hatarini kutumbukia tena katika baa la njaa wakati ambapo watu milioni tano au zaidi ya wakaazi wanne kati ya kumi, hawana chakula cha kutosha.

Mapigano kati ya al-Shabaab na serikali ya Somalia injayoungwa mkono na Umoja wa Afrika yanaendelea, ambapo siku ya Jumatano watu 28 waliuawa katika shambulio lililofanyika katika mji mkuu Mogadishu.

Wanejshi wa Somalia na AU wamewafurusha Al-Shabaab kutoka ngome zao kuu mijini na bandari, lakini mara nyingi wamepambana kuyalinda maeneo madogo ya mbali dhidi ya mashambulizi.

Maelfu ya Wasomali wanatoka sehmu moja kwenda nyingine wakisaka chakula na maji, wengi wao wakivuka mipaka na kuingia nchini Ethiopia ili kupata, yanasma mashirika ya hisani.

Dürre ohne Ende Am Horn von Afrika droht Hungersnot
Somalia imekuwa ikikumbwa na njaa mara kwa mara kutoka na ukame unaojirudia.Picha: picture-alliance/dpa

Save the Children inasema kuna viwango vikubwa vya utapiamlo miongoni mwa watoto iliowafanyia vipimo baada ya kuwasili katika kambi kubwa ya Dollo Ado nchini Ethiopia.

Wasomali wengi wamekuwa wakiishi uhamishoni kwa miongo mitatu ambapo karibu milioni moja wanaishi katika kambi za wakimbizi zilizoko katika mataifa jirani ya Ethiopia, Kenya, Djibouti na Uganda, ambako pia chakula kimekuwa shida kutoka na kupungua kwa ufadhili.

Nchini Ethiopia, ambayo iliathirika vibaya na ukame mwaka 2016, karibu watu milioni sita wanahitaji msaada wa chakula na zaidi ya milioni moja wanashinda njaa nchini Kenya, na idadi hiyo inatarajiwa kuongegezka katika miezi ijayo.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/rtre

Mhariri: Saumu Yusuf