Kati ya mambo yanayotajwa kuchangia ujauzito wa wasichana shuleni ni pamoja na elimu duni ya afya ya uzazi, ikiwemo elimu juu ya mabadiliko ya miili kwa wasichana. Kipindi cha Wanawake na Maendeleo kinaangazia mpango wa kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi wa kike Tanzania. Msikilize Celina Mwakabwale katika makala.