MigogoroSudan
Watu 127 wauawa kufuatia mapigano nchini Sudan
11 Desemba 2024Matangazo
Karibu watu 60 wameuawa katika mji wa Omdurman huku wengine zaidi ya 100 wakiuawa katika soko la Kaskazini mwa mji wa Kabkabiya huko Darfur.
Gavana wa Khartoum, Ahmed Othman Hamza, amesema kombora lililorushwa na RSF lilipiga basi la abiria na kuwaua watu wote 22 waliokuwamo ndani.
Pande hizo mbili ambazo zimekuwa zikipambana tangu Aprili mwaka 2023, zimeshutumiwa kushambuliana vikali kwa makombora na kuyalenga maeneo ya raia yanayokaliwa na watu wengi.