JangaBrazil
Watu 22 wapoteza maisha ajali ya basi nchini Brazil
21 Desemba 2024Matangazo
Maafisa wa jimbo hilo wamesema ajali hiyo ilitokea pale basi hilo la abiria lilipopasuka tairi na kupoteza mwelekeo na kisha kugongana na lori la mizigo mnamo majira ya asubuhi kwa saa za Brazil. Inaarifiwa chombo hicho kilikuwa kimewabeba abiria 45 kilipoondoka mji wa Sao Paulo mnamo alfajiri.
Taarifa ya idara ya zimamoto wa jimbo la Minas Gerais wamesema baada ya jitihada ya saa kadhaa walifanikiwa kuuzima moto na kuipata miili ya watu 22 waliokwama ndani ya basi na kutetekea. Idara hiyo pia imesema watu wengine 13 wamejeruhiwa na wamepelekwa kwenye hospitali ya mji jirani.