1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 3 wajeruhiwa kufuatia shambulizi la bomu Ukraine

16 Januari 2024

Watu watatu wamejeruhiwa na majengo sita ya ghorofa yameharibiwa baada ya Urusi kufanya shambulio la kombora katika mji wa New York, mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4bJ88
USA New York | Volodymyr Zelenskyj, rais wa Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine imeeleza kuwa, watu wengine watano wamenasa chini ya vifusi.

Picha zilizochapishwa na wizara hiyo zimeonyesha waokoaji wakiendelea na zoezi la kutafuta manusura katika kile kilichoonekana kuwa sehemu ya gorofa iliyoporomoka.

Ukraine imeshuhudia ongezeko kubwa la vifo vya raia tangu Disemba mwaka jana, baada ya Urusi kuzidisha mashambulizi ya anga, tofauti kabisa na hali ilivyokuwa mapema mwaka 2023.

Mji wa New York, ulioko katika eneo la Donetsk mashariki mwa Ukraine, umejikuta katika mstari wa mbele wa mbele wa vita kati ya vikosi vya Ukraine na makundi yanayotaka kujitenga na ambayo yanaungwa mkono na Urusi.