Watu 854 wamekufa India
30 Julai 2005Matangazo
Bombay:
Waokoaji nchini India wamegundua maiti nyingine za watu waliofariki kutokana na mvua kubwa za masika. Idadi ya watu waliofariki magharibi mwa India mpaka sasa ni 853. Wanajeshi, Wapiga mbizi wa jeshi la majini na Waokoaji wamekuwa wakiwatafuta Wahanga baada ya mvua kubwa na matope kuikumba sehemu kubwa ya mkoa wa Maharashtra mapema juma hili. Maiti zaidi ya 100 zimepatikana katika wilaya ya Raigarh karibu na Bombay. Afisa wa mkoa wa Maharastra, Vishnu Patil, amesema kuwa idadi ya watu waliofariki imefikia 853 na huenda ikaongezeka zaidi. Ameongeza kusema kuwa watu wengi wameuawa na milima ya matope iliyowafunika.