1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 9 wauwawa kwenye shambulizi la bomu nchini Somalia

4 Januari 2023

Idadi ya vifo kutokana na miripuko miwili iliyotokea Somalia mapema leo imeongezeka na kufikia watu 19.

https://p.dw.com/p/4LjsB
Symbolbild I Über 100 Tote bei Terrorangriff in Mogadischu
Picha: Farah Abdi Warsameh/AP/dpa/picture alliance

Hayo ni kulingana na duru ya kiusalama. Watu wengine kadhaa walijeruhiwa kufuatia mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotokea kwa wakati mmoja katika mji wa Mahas ulioko eneo la kati nchini Somalia.

Abdullahi Adan, afisa wa usalama wa mji huo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "magaidi walishambulia mji wa Mahas asubuhi ya leo kwa kutumia mabomu yaliyotegwa kwenye magari."

Shambulizi hilo ambalo limedaiwa kufanywa na wanamgambo wa Al Shabaab limetokea katika jimbo la Hiram, ambako miezi kadhaa iliyopita operesheni kali ilifanywa dhidi ya kundi hilo lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda.