Watu saba wafa kwenye maporomoko ya udongo Uganda
26 Mei 2023Matangazo
Kulingana na mkuu wa wilaya hiyo Stanley Bayola mvua hiyo iliyoandamana na upepo mkali ilinyesha kwa muda wa saa saba na kusababisha uharibifu mkubwa kwa makazi na mashamba ya watu wa eneo hilo.
Juhudi za kufukua maiti za wahanga na pia kuwanusuru baadhi ya watu waliokwama katika vifusi zinaendelea kwa sasa.
Maporomoko yaua watu 34 Uganda
Inahofiwa kuwa idadi ya waliopoteza maisha yao inaweza kuongezeka kutokana na mazingira magumu ya kuwafikia watu wa familia kadhaa ambazo njia yao ya kujinusuru inazidi kuwa ngumu.
Visa kama hivyo vya maporokomo ya ardhi na tope hutokea mara kwa mara eneo hilo na watu hushauriwa kuchukua tahadhari katika msimu wa mvua. Ila kwa wengi ni vigumu kwao kuyahama makazi yao ya muda mrefu.