SiasaChina
Watu saba wauawa California ikiomboleza shambulizi la tatu
24 Januari 2023Matangazo
Mkasa huo ni wa tatu wa mauaji ya watu wengi kufanyika katika jimbo hilo ndani ya siku nane, likiwemo shambulizi lililotokea kwenye ukumbi moja wa densi ambalo lilisababisha vifo vya watu 11 wakati wa maadhimisho ya Mwaka mpya wa Kichina.
Maafisa walimkamata mshukiwa wa mashambulizi ya jana, Chunli Zhao mwenye umri wa miaka 67, baada ya kumkuta ndani ya gari kwenye eneo la kuegesha magari.Watu wanne walipatikana wamekufa na wa tano akiwa na majeraha ya risasi kwenye shamba moja.
Maafisa waliwapata watu wengine watatu wakiwa wameuawa kwenye eneo jingine mbali kidogo na lilikotokea shambulizi la kwanza. Polisi wamesema bado hawajabaini lengo la shambulizi hilo.