1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wawili wameuwawa katika shambulio la Urusi Ukraine

26 Agosti 2023

Maafisa wa Ukraine wamesema watu wawili wameuwawa na mmoja amejeruhiwa katika shambulio kwenye eneo la Podoli Mashariki mwa mji wa Kupyansk.

https://p.dw.com/p/4VbvK
Ukraine Krieg | Ukrainische Soldaten an der Front bei Bachmut
Picha: Genya Savilov/AFP/Getty Images

Gavana wa Kharkiv Oleh Synehubov amesema mgahawa uliokuwa na wakaazi wengi mjini humo, ulishambuliwa na adui.

Wanajeshi wa Urusi wameimarisha juhudi zao za kijeshi katika eneo hilo kama sehemu ya kupambana na mashambulizi kutoka Ukraine Kusini mwa taifa hilo. 

Urusi yadungua droni mbili zilizolenga Moscow

Wanajeshi hao hivi karibuni wamezidi kujiimarisha Kaskazini Mashariki mwa Ukraine.Shambulio la Kupyansk limethibitisha tathimini ya wizara ya ulinzi ya Uingereza iliyosema kwamba Urusi inaweza kulishambulia zaidi eneo hilo.