JamiiZambia
Wawili wazuiwa Zambia kwa kutaka kumdhuru rais "kishirikina"
21 Desemba 2024Matangazo
Msemaji wa polisi Rae Hamoonga alisema katika taarifa kwamba watuhumiwa hao wawili, Jasten Mabulesse Candunde, na Leonard Phiri, wanadaiwa kutumwa na Nelson Banda, mdogo wa mbunge anayekabiliwa na tuhuma za wizi Jay Jay Banda, kumroga kiongozi huyo wa Malawi.
Madai dhidi yao ni kufanya uchawi, kumiliki hirizi na ukatili kwa wanyama baada ya kukutwa na hirizi za aina mbalimbali zikiwemo
kinyonga hai na wanadaiwa kuwa ni waganga.
Msemaji wa polisi amesema watuhumiwa hao walisema kwamba walikubaliana kulipwa dola 7,400 kwa kazi hiyo.