Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Sylvester Ilunga Ilunkamba amekubali kujiuzulu. Tangazo hilo kalitoa saa chache tu kabla ya kutimia muda wa saa 24 aliopewa na bunge kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Félix Tshisekedi. Baada ya kura na bunge ya kutokuwa na imani naye Ilunkamba alikataa kujiuzulu akipinga uhalali wake. Jean Noel Ba-Mweze alituarifu.