Tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka 2019 yatunukiwa waziri mkuu Abiy Ahmed wa Ethiopia kwa juhudi zake za kuupatia ufumbuzi mgogoro wa mpaka kati yake na Eritrea. Tuzo hiyo imelifanya bara la Afrika kugonga vichwa vya habari duniani.Na chama cha upinzani huko Tanzania Chadema chaitaka serikali imuhakikishia usalama wake aliyekuwa mbunge wa chama chake,Tundu Lissu.Yote hayo ni katika Afrika wiki hii.