Waziri Mkuu wa India Vajpayee aizuru Pakistan
4 Januari 2004Matangazo
ISLAMABAD: Kwa mara ya mwanzo tangu miaka mitano Waziri Mkuu wa India Atal Bihari Vajpayee amewasili nchiniPakistan. Ziara yake hiyo inasemekana inatoa nafasi ya kihistoria ya kutengeneza uhusiano uliokorofeka kati ya India na Pakistan. Mkoa wa Kashmir ni kiini cha mvutano huo wa miaka mingi kati ya madola hayo mawili ya kinyuklea. Lakini haijadhihirika iwapo Waziri Mkuu wa India Vajpaye atakutana na Rais wa Pakistan Pervez Musharraf wakati wa ziara hii. Bwana Vajpayee anahudhuria Mkutani wa Kilele wa Mataifa ya Asia ya Kusini unaoanza hii leo mjini Islamabad. Mkutano huo unahudhuria pia na viongozi kutoka Bangladesha, Sri Lanka, Nepal, Bhutan na Malediva.