Waziri Faeser aionya AfD kutotumia shambulio la Magdeburg
26 Desemba 2024Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Nancy Faeser, amekionya chama cha mrengo mkali wa kulia, cha Alternative for Germany (AfD), dhidi ya kutumia shambulio la soko la Krismasi Magdeburg kwa manufaa ya kisiasa, akisema ni kitendo cha kusikitisha na cha aibu.
Soma pia: Ujerumani yachunguza maonyo kuhusu muuaji wa soko la Krismas
Baada ya shambulio hilo, ambalo liliua watu watano na kujeruhi zaidi ya 200, AfD iliandaa maandamano yaliyohudhuriwa na takriban watu 3,500, ambapo mwenyekiti wake Alice Weidel alitumia tukio kuhamasisha wafuasi wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu, huku zikisikika kauli za "Fukuza! Fukuza!"
Uchunguzi dhidi ya daktari huyo mwenye asili ya Saudi Arabia, aliyefika Ujerumani mwaka 2006 na kupatiwa hadhi ya ukimbizi, bado unaendelea.