1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa michezo wa Afrika kusini

Ramadhan Ali17 Agosti 2007

Anasema kombe la kwanza la dunia la dimba 2010 litaifufua Afrika katika macho ya walimwengu.

https://p.dw.com/p/CHbG

Waziri wa michezo wa Afrika Kusini, anaamini kwamba Kombe la dunia la kwanza kuaniwa barani Afrika 2010, litalifufua bara la Afrika ulimwenguni.

Mfumo mpya kuanzishwa katika Bundesliga-ligi ya Ujerumani ambamo timu ya tatu ya mwisho katika timu za daraja ya kwanza, itabidi kucheza na timu ya tatu katika daraja ya pili ili kuania nafasi ya kucheza daraja ya kwanza.Na kwa mara ya kwanza tangu ashike usukani wa Holland, kocha Marco van Basten amemuita Ruud Van Nistelrooy kujiunga na kikosi cha taifa kitakachocheza na Uswisi, jumatano ijayo mjini Geneva.

Waziri wa michezo wa Afrika Kusini Makhenkhesi Stofile anaamini kwamba kuandaa kombe la kwanza la dunia barani Afrika 2010,kutapalilia ulimwengu kuonesha shauku mpya juu ya bara hilo.

Stofile akasema changamoto kubwa inayolikabili bara la Afrika ni jinsi gani ya kuvutia faida zinazotokana na mashindano hayo makubwa ya dunia mara tu firimbi ya mwisho ikilia.

Nae mwenyekiti wa ushirika wa mawasiliano ya kitaifa NCP kwa kombe la dunia 2010,Nkenke Kekana

Alisema, „tunahitaji kutumia fursa hii ili kutoa sura njema kwa bara letu.“Akaongeza kusema kombe la dunia barani afrika ni zaidi ya kucheza dimba pekee.Inahusu pia juu kukua kwa uchumi na maendeleo ya bara la Afrika.

Mfumo mpya utaanzishwa ili kuichangamsha zaidi Bundesliga-Ligi ya Ujerumani .Kuanzia msimu wa mwakani timu ya 3 ya mwisho katika orodha ya ligi ya daraja ya pili itacheza na ile ya tatu katika ngazi ya daraja ya pili kuamua nani anacheza katika daraja ya kwanza.

Mtindo wa hivi sasa ni kuwa timu 3 za mwisho za daraja ya pili zinateremshwa daraja ya 3 wakati 3 bora za daraja ya pili zapanda daraja ya kwanza.

Ruud van Niestelrooy,mshambulizi hatari aliehamia Real madrid kutoka Manchester United,kwa mara ya kwanza atvaa tena jazi ya timu ya taifa ya Holland chini ya kocha Marco van Basten.Mara ya mwisho Niestelrooy, kuichezea Holland ilikua ilipotoka sare 0:0 na Argentina katika kombe la dunia Juni,mwaka jana.