Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Korea
21 Aprili 2007Matangazo
SEOUL:
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung leo alizuru eneo linalokatazwa mapigano linalogawa Korea ya kusini kutoka ile ya kaskazini.Baadae aliruka kurejea Ujerumani baada ya kumaliza ziara yake ya Asia ilioingiza China na Japan.
Alipokuwa mpakani kati ya korea hizo mbili, Bw.Jung alisema imemkumbusha hali ilivyokua nchini Ujerumani kabla nchi mbili za Ujerumani-mashariki na magharibi kuungana.