SiasaPakistan
Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Pakistan akamatwa
2 Februari 2023Matangazo
Waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Pakistani na mshirika wa kiongozi aliyeondolewa madarakani, Iman Khan, amekamatwa leo Alhamisi, masaa machache baada ya kiongozi mwingine mkuu wa upinzani kuachiliwa kutoka kizuizini.
Sheikh Rashid Ahmed, ambaye anaongoza chama kilichokuwa katika muungano na Khan, alifikishwa katika mahakama ya Islamabad ambapo amepelekwa rumande kwa siku mbili.
Kulingana na nyaraka za mashtaka, Ahmed anashikiliwa kutokana na matamshi aliyoyatoa dhidi ya rais wa zamani, Asif Ali Zardari, akimtuhumu kwa kupanga njama ya kumuua waziri mkuu wa zamani, Imran Khan.
Khan na viongozi wengine wa chama chake wamekuwa wakikabiliana na kesi kadhaa mahakamani, jambo ambalo wengi wanachukulia kuwa mbinu dhidi yao.