1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: homa ya kuku kudumu miaka kadha

15 Februari 2004
https://p.dw.com/p/CFgZ
HANOI: Shirika la Afya la Kimataifa, WHO limesema uko uwezekano kuwa mapigano dhidi ya homa ya kuku yataendelea kudumu miaka kadha. Nalo Shirika la Chakula la Kimataifa, FAO linakhofia kwamba homa hiyo ya kuku itaendelea kuwa kitisho kwa miaka kadha. Huko Thailand, kaskazini-Mashariki mtoto wa miaka 13 amefariki kutokana na homa hiyo. Pia inasemekana kuna kisa cha kuambukizwa mtoto wa Kithai mwenye umri wa mwaka mmoja. Nchini Uchina ugonjwa huo wa kuambukiza wa homa ya kuku umejitokeza katika mashamba manne ya ufugaji wa kuku kwenye mkoa wa Kusini Guangdong na eneo jirani Guangxi, liliripoti shirika la habari la Uchina, XINHUA. Hivi sasa yamekwisha athirika jumla ya mashamba 34 ya kuku nchini Uchina, wakati ziko shutuma za kuambukizwa mashamba 13 mengine.