WHO yaendelea na uchunguzi wa ugonjwa usiojulikana Kongo
9 Desemba 2024Matangazo
Ugonjwa huo ulilipuka tangu mwezi wa Oktoba mwaka huu.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema katika taarifa yake kwamba watu hao zaidi ya 400 wamekumbwa na maradhi hayo na 31 wamekufa kwenye jimbo la Panzi, lililoko umbali wa zaidi ya kilomita 700 kutoka mji mkuu, Kinshasa.
Wizara ya afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeripoti vifo kadhaa vilivyotokea nje ya vituo vya afya na imesema vifo hivyo vinahitaji kuchunguzwa na shirika hilo la afya ulimwenguni.
Dalili za ugonjwa huo, usiojulikana, ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa, kikohozi, mafua na maumivu ya mwili.