1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wito kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu Kenya

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyJG

NAIROBI: Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan ametoa wito wa kufanywa uchunguzi kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu nchini Kenya.Annan yupo Kenya akijaribu kuleta masikilizani kati ya Rais Mwai Kibaki na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.Annan amesema,mzozo wa nchini Kenya sasa si tena mgogoro unaohusika na matokeo ya uchaguzi.

Siku ya Alkhamisi,Annan alifanikiwa kuwakutanisha Kibaki na Raila kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa Desemba uliozusha mabishano.Odinga na wafuasi wake na hata wasimamizi wa kimataifa wanasema,uchaguzi huo ulitiwa doa kwa mambo yasiokuwa ya kawaida.

Takriban watu 800 wameuawa na zaidi ya laki mbili na nusu wengine wamekimbia makaazi yao kufuatia machafuko yaliyozuka baada ya Kibaki kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa rais.