1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wito wa ODM kuandamana kwa amani Alkhamisi ijayo

20 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cv0Q

NAIROBI: Mapambano mapya ya kikabila yalizuka usiku wa jana katika eneo la mabanda la Mathare mjini Nairobi.Watu 2 wamepoteza maisha yao katika machafuko hayo.Juma hili,si chini ya watu 38 waliuawa katika maandamano ya siku tatu,kufuatia hatua kali zilizochukuliwa na polisi.Chama cha upinzani cha ODM kinapinga matokeo ya uchaguzi wa mwezi Desemba ambao ulimrejesha tena madarakani Rais Mwai Kibaki.Upinzani unadai kuwa uchaguzi huo ulifanyiwa udanganyifu.

Siku ya Jumamosi,Henry Kosgey alie mwenyekiti wa chama cha ODM aliuambia mkutano wa waandishi wa habarimjini Nairobi kuwa Alkhamisi ijayo,kote nchini kutafanywa maandamano ya amani.Azma ni kuendelea na kampeni ya kuishinikiza serikali kuchukua hatua ya kutenzua mgogoro unaohusika na uchaguzi.

Wakati huo huo,Kamishna wa Maendeleo wa Umoja wa Ulaya,Louis Michel amekuwa na mikutano mbali mbali pamoja na Rais Mwai Kibaki na kiongozi wa chama cha upinzani-ODM bwana Raila Odinga.Baadae akasema kuwa Kibaki yupo tayari kukutana na Odinga katika jitahada ya kupata ufumbuzi wa mgogoro unaohusika na matokeo ya uchaguzi.