Wolfsburg ndani, Moenchengladbach nje
9 Desemba 2015Manchester United wakicheza ugenini dhidi ya VfL Wolfsburg ilisalimu amri baada ya kupata kichapo cha 3-2 na kuondolewa katika michuano hiyo,
Manchester City wakiwa nyumbani Etihad waliwavunja moyo Borussia Moenchengladbach wa Ujerumani kwa kupata ushindi wa 4-2 mabao ambayo yamefungwa na David Silva, Raheem Sterling na Bony Wilfried. Ushindihuo uliwaweka kileleni mwa kundi D.
Vinara wa kundi A Timu ya Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu waliwazaba Malmo kutoka Sweden mabao 8-0 ambayo yalingwa na wachezaji karim Benzema mabao (3), Christiano Rolnado mabao (4) pamoja na Mateo kovacich bao (1).
PSG ya Ufaransa iliizidi nguvu Shakhtar Donetsk ya Ukraine kwa kuifunga 2-0, kupitia wachezaji Lucas Moura na Zlatan Ibrahimovic.
Michezo mingine PSV Eindhoven imeichapa 2 – 1 CSKA Moskova, Benfica ikalazwa 1 – 2 na Atletico Madrid, Galatasaray imetoka sare ya 1 – 1 na FC Astana, huku Sevilla ikishinda bao 1 – 0 dhidi ya Juventus.
Mechi hizo za makundi zitaendelea tena zinatarajia kuendelea tena hii leo kwa michezo mbalimbali ,na miongoni mwa mechi hizo niBayer Leverkusen na Barcelona, Olympiakos na Arsenal, Dinamo Zagreb na Bayern Munichi.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef