Wolfsburg yaomboleza kifo cha Malanda
11 Januari 2015Mkurugenzi wa Michezo wa Klaus Allofs amesema haukuwa uamuzi rahisi wa kufanya lakini timu hiyo itaondoka Ujerumani baadaye leo baada ya kufuta safari yao jana jioni kufuatia habari za kifo cha Malanda.
Kiungo huyo aliyekuwa na umri wa miaka 20 alikuwa katika kiti cha nyuma cha gari akisafiri kujiunga na wenzake jana mchana wakati gari hilo lilipougonga mti. Watu wengine wawili waliokuwemo ndani ya gari hilo walinusurika.
Kocha Dieter Hecking alitiririkwa na machozi katika kikao cha waandishi wa habari wakati akisema kifo cha Malanda kimewacha “shimo kubwa“. Wolfsburg wataendelea na mipango yao ya kucheza mechi mbili za kirafiki nchini Afrika KUSINI wakati timu hiyo ikijiandaa kwa mzunguko wa pili wa Bundesliga unaoanza mwishoni mwa mwezi huu. Mamia ya mashabiki wa klabu hiyo walikusanyika jana usiku katika uwanja wao wa Volskwagen Arena, wakiomboleza kwa kuwasha mishumaa na kuweka mauwa.
Mwandishi. Bruce Amani/Reuters
Mhariri: Mohamed Dahman