Schürrle aipa Wolfsburg tikiti ya hatua ya mchujo
26 Novemba 2015Timu hiyo ya Uhispania tayari ilikuwa imefuzu katika hatua ya 16 za mwisho. Paris Saint Germain ilipata ushindi wa tano bila dhidi ya Malmo huku mshambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahimovic akifunga goli la tatu dhidi ya klabu hiyo ya Sweden aliyowahi kuichezea zamani.
Juventus iliiruka Manchester City na kukamata nafasi ya kwanza katika Kundi D kwa kupata ushindi wa moja bila mjini Turin. Seville ilizabwa mabao manne kwa mawili na Borussia Moenchengladbach wakati Wolfsburg wakiweka guu moja kwenye duru ya mchujo baada ya kusajili ushindi wa mbili sifuri ugenini dhidi ya CSKA Moscow. Manchester United ilifurukuta na kutoka sare ya bila kufungana nyumbani na wageni PSV Eindhoven.
Kwingineko FC Astana imetoka sare ya bao 2-2 na Benfica, Atletico Madrid imeifunga Galatasaray bao 2-0.
Timu zilizojihakikisha tikiti ya awamu ya mchujo ni:
Real Madrid
Paris St-Germain
Atletico Madrid
Benfica
Juventus
Manchester City
Barcelona
Bayern Munich
Zenit St Petersburg
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Josephat Charo