Katika michuano ya AFCON inayoendelea nchini Misri, hapo jana Madagascar ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza iliendeleza miujiza yake kwa kuibandua Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wakati huo huo kuna wimbi linaloendelea la makocha kufungishwa virago, pale timu zao zinapoyaaga mashindano hayo hayo. Sikiliza mahojiano haya kati ya Daniel Gakuba na mchambuzi wa masuala ya soka, Mtemi Ramadhan