1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yanga ya Tanzania kushuka dimbani ligi ya mabingwa Afrika

7 Desemba 2024

Mechi za pili za hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika CAFzinaendelea leo katika viwanja mbalimbali barani Afrika. Mabingwa wa ligi kuu soka ya Tanzania Yanga watashuka dimbani kucheza na MC Alger.

https://p.dw.com/p/4nsAd
| Young Africans - USM Alger
Kipa wa Yanga Diarra katika heka heka ya kulinda langoPicha: Sports Inc/empics/picture alliance

Mechi za pili za hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika CAF zinaendelea leo katika viwanja mbalimbali barani Afrika. Mabingwa wa ligi kuu soka ya Tanzania Yanga watashuka dimbani kucheza na MC Alger ugenini majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Soma zaidi: Droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika yafanyika Cairo

Yanga ambayo ni mwakilishi pekee kutoka Tanzania katika ligi ya mabingwa Afrika inahitaji kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri baada ya kupoteza katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Al Hilal ya Sudan mjini Dar es Salaam.

Michezo mingine ya michuano hiyo ni kati ya FAR Rabat ya Morocco dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Orlando Pirates ya Afrika Kusini pia dhidi ya Al Ahly ya Misri.