Zambia
23 Agosti 2008Matangazo
Lusaka
Serikali ya Zambia imesema mazishi ya marehemu rais Levy Mwanawasa yatafanyika September tatu ijayo.Katibu wa baraza la mawaziri Dr. Joshua Kangaja amesema tarehe hiyo inasadif na siku Mwanawasa aliyozaliwa.Angekua hai,angekamilisha umri wa miaka 60.Maiti ya marehemu rais Levy Mwanawasa inataraajiwa kuwasili nyumbani mjini Lusaka leo hii kutoka Paris.Alifariki dunia akiwa katika hospitali mashuhuri ya mjini Paris ,kwa matibabu ya kiharusi Agosti 19 iliyopita.Kwa mujibu wa waziri wa sheria wa Zambia,uchaguzi wa rais utaitishwa siku 90 baada ya kifo cha rais,kama inavyotakikana kikatiba.