Migogoro
Zelensky: Wanajeshi wengi wa K.Kaskazini wanapambana Kursk
15 Desemba 2024Matangazo
Rais Zelensky amesema hayo jana usiku katika ujumbe wa video, na kuongeza kuwa uharibifu ni mkubwa, ingawa hakueleza zaidi.
Zelensky amemshutumu Rais Vladimir Putin kwa kuchochea vita kwa makusudi dhidi ya Ukraine na kupuuza miito kutoka China na Brazil ya kufanya kila linalowezekana kupunguza mzozo.
Kiongozi huyo aidha, ametangaza nia yake kushirkiana na Syria, akisema kuna umuhimu mkubwa kwa nchi hiyo kurejea kwenye utulivu kwa haraka, ili ulimwengu ujikite katika kurejesha amani nchini Ukraine.