1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky asifu kusimama kwa usambazaji gesi ya Urusi

Sylvia Mwehozi
2 Januari 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesifu kusimamishwa kwa usafirishaji wa gesi ya Urusi katika mataifa ya Ulaya kupitia nchi yake.

https://p.dw.com/p/4okAV
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: John Thys/AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesifu kusimamishwa kwa usafirishaji wa gesi ya Urusi katika mataifa ya Ulaya kupitia nchi yake akisema ni hatua ya kushindwa kwa Moscow katikati mwa uvamizi wake wa karibu miaka mitatu.

Usambazaji wa gesi ya Urusi kwa mataifa ya Ulaya kupitia Ukraine, umesimamishwa jana baada ya Zelensky kukataa kurefusha ushirikiano wa miongo kadhaa ambao umekuwa na manufaa kwa mataifa yote mawili. Zelensky alimnyooshea kidole moja kwa moja Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuvunjika kwa ushirikiano huo.

Ukraine ilizishambulia nchi ambazo bado zinanunua gesi kutoka Urusi ikisema kuwa zinaisaidia Moscow mapato kuendesha vita vyake. Urusi imesema Ukraine inajiongezea matatizo na kuwakatisha tamaa washirika wake wa Ulaya mashariki ambao wanategemea usambazaji wa Urusi. Uamuzi wa Ukraine umepokelewa kwa hisia tofauti Ulaya.