1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky awasifu raia wa Ukraine kwa kupambania uhuru

24 Agosti 2023

Rais Volodymyr Zelensky amewasifu watu wa taifa hilo kwa kupambania uhuru wao katika hotuba yake aliyotoa Alhamis kwenye maadhimisho ya pili ya uhuru wa Ukraine kufanyika ikiwa imevamiwa na Urusi.

https://p.dw.com/p/4VXKR
Ukraine | Krieg | Tag der Nationalflagge und Gipfeltreffen der Krim-Plattform in Kiew
Picha: President Of Ukraine/ZUMAPRESS/picture alliance

Zelensky amesema kupitia mitandao ya kijamii kwamba uhuru ni kitu cha muhimu kwa kila mmoja na wanatakiwa kuupambania.

Mkuu wa ujasusi wa jeshi, Kyrylo Budanov, amesema kupitia mtandao wa Telegram kwamba mapambano ya uhuru bado yanaendelea, huku mkuu wa usalama wa taifa, Vasyl Maliuk, akiandika sikukuu kama ya leo imekuwa na maana mpya, kutokana na vita hivyo vinavyotimiza miezi 19.

Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen, amewasifu raia kwa ujasiri, nguvu na matumaini ya kudumu kuelekea mustakabali wa amani na ustawi wa Ulaya iliyo moja.